Wikipedia

Nairobi

Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Nairobi_Skyline2.jpg: Nite Owl derivative work: Jjtkk · CC BY 3.0

page banner

Nairobi_Skyline2.jpg: Nite Owl derivative work: Jjtkk · CC BY 3.0

Nairobi banner.jpg

Nairobi ni mji mkuu na jiji kubwa zaidi la Kenya, lililoko katika sehemu ya kusini-kati ya nchi. Jina lake limetokana na usemi wa Kimaasai "Enkare Nairobi," maana yake "maji baridi," likirejelea Mto Nairobi unaopita katikati ya jiji. Kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa takriban milioni 4.5 ndani ya jiji na zaidi ya milioni 10 katika eneo la mji mkuu(Metro), Nairobi ni kitovu kikuu cha uchumi katika Afrika Mashariki. Inahudumu kama kituo muhimu cha kifedha, biashara, na usafiri, ikiwa na makao makuu ya mashirika mengi ya kimataifa, kampuni za kimataifa, na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili pamoja na Sheng.

sw.wikipedia.org · 211

Sanamu ya Jomo Kenyatta. W

Jiografia

coordinate location -1.28639, 36.8172 W

coordinate location

locator map image
Nairobi123 · CC BY-SA 3.0

locator map image

Nairobi123 · CC BY-SA 3.0

Nairobi County location map.png

ipo katika eneo la kiutawala
Kaunti ya Nairobi
Jorge Láscar · CC BY-SA 2.0
sehemu ya
Southern Rift Valley
WUser:Chris 73 · CC BY-SA 3.0
elevation above sea level
1661 mita
W

jina

sw

jina rasmi
NairobiW
native label
NairobiW
demonym
Nairobian en+

en

jina rasmi
NairobiW sw+
native label
NairobiW sw+
demonym
Nairobian

eo

jina rasmi
NairobiW sw+
native label
NairobiW sw+
demonym
Najrobiano

fr

jina rasmi
NairobiW sw+
native label
NairobiW sw+

tn

jina rasmi
NairobiW sw+
native label
NairobiW sw+
demonym
Monairobi

pronunciation audio

Kiswahili
Picha ya nembo ya taifaW
Josedar (SVG conversion) · CC BY-SA 4.0

Picha ya nembo ya taifa

Josedar (SVG conversion) · CC BY-SA 4.0

Coat of Arms of Nairobi.svgW

picha ya bendera
earlier version Mandingoesque; this version Johannes Rössel · Public domain

picha ya bendera

earlier version Mandingoesque; this version Johannes Rössel · Public domain

Flag of Nairobi.svg

msimbo wa posta
00100
local dialing code
020
W

serikali

mkuu wa serikali

mji mkuu wa former
Koloni ya kenya 1920 – 1963

mji mkuu wa 3

demografia

Nchi: Kenya

idadi ya watu11 %
area0.12 %

elevation above sea level(mita) big city· Kenya · 3 / 5

idadi ya watu namba ya watu katika eneo fulani

muda wa tukio idadi ya watu
20093138369
20103240155
20165545000
area
696 kilomita ya mraba
W

uchumi

economy of topic
economy of Nairobi

relation

twinned administrative body 7

historia

kuanzishwa

Historia

Chanzo kwenye kambi la reli

Nairobi ilianzishwa na Waingereza mwaka 1899 kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Njia ya reli ilikuwa imefika kutoka Mombasa ikaonekana ya kwamba kuanzia hapa kasi ya ujenzi itachelewa kutokana na ugumo na eneo la Bonde la Ufa na mitelemko yake mikali. Mahali palikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji pakaonekana panafaa kwa kituo njiani. Hasahasa ilionekana tabianchi ya nyanda za juu ilifaa kiafya kwa Waingereza walioteswa na joto la pwani na kwenye nyanda za chini.

Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa mwaka 1896 kando ya mto Nairobi na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri wafanyakazi wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata 1897 wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye.

Mji mkuu wa koloni

Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe 30 Mei 1899. Hapo idadi ya wafanyakazi - hasa Wahindi - iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya mahema na ghala za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya mabati ilifika kutoka Mombasa - tayari kwa reli - na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la kituo cha reli cha leo. Mwezi wa Agosti kamishna Mwingereza wa jimbo la Ukamba aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka Machakos akajenga boma lake kwenye eneo la Moi Avenue, mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya polisi ya kihistoria yanayotazama Bustani ya Jivanji.

Barabara kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa huko kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.

Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya mvua kali sehemu ya mahema na vibanda vilipatikana katikati ya ziwa la matope. Magonjwa yalisambaa na baada ya epidemia ya tauni soko la Wahindi Lilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye kilima cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill.

Mwaka 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa, baadaye Kenya Colony).

Uchumi wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na utalii; matajiri wengi kutoka pande zote za dunia waliFIka kwa kusudi la kuwinda wanyama wakubwa wakivutwa na wingi wa wanyama kwenye nyanda za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi katika mazingira ya mji ilitolewa kwa walowezi Wazungu na kilimo cha biashara kilianza kuchangia.

Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa mabweni ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao.

Lakini Waingereza waliajiri askari kutoka Sudan na Somalia katika jeshi na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. Wapagazi na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji wenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo 1921 kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani.

Tangu uhuru

Mwaka 1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya ikaendelea kukua haraka.

en.wikipedia.org

Timeline of Nairobi

multimedia

nighttime view
Africanmodern · CC BY-SA 4.0

nighttime view

Africanmodern · CC BY-SA 4.0

Nairobi economic capital of africa.jpg

montage image
Southlondoneye (talk) 20:30, 29 March 2015 (UTC) · CC BY-SA 3.0

montage image

Southlondoneye (talk) 20:30, 29 March 2015 (UTC) · CC BY-SA 3.0

Nairobi Montage A.jpg

aerial view
Mkimemia at English Wikipedia · Public domain

aerial view

Mkimemia at English Wikipedia · Public domain

Nairobi Aerial Photo.jpg

Video 29 MB
Google Earth · CC BY 3.0

Video

Google Earth · CC BY 3.0

Google Timelapse- Nairobi, Kenya.webm · 29 MB

Jamii ya vitu vya kawaida
Nairobi
Commons gallery
Nairobi
W

Eneo la jiji la Nairobi

Kaunti ya Nairobi (nyekundu) ndani ya jiji kuu la Nairobi (kijani).

Nairobi yenyewe iko ndani ya eneo la jiji la Nairobi (kwa Kiingereza: Greater Nairobi Metropolitan region) lililoundwa na kaunti 4 kati ya jumla ya 47 za Kenya.

Kaunti hizo ni:

Chanzo: Kenya Census

Eneo hilo linazalisha asilimia 60 za pato la taifa.

Mazingira na hali ya hewa

Nairobi iko kilomita 150 upande wa kusini ya ikweta kwenye nyanda za juu za Kenya kando la mto Nairobi. Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya mto Athi inaanza kupanda juu hadi milima ya Ngong na vilima vingina vinyvyofanya ukuta wa mashariki wa Bonde la Ufa.

Kitovu cha Nairobi kiko zipatao m 1624 juu ya UB. Sehemu za mashariki za jiji ziko bado kwenye tambarare, na sehemu za magharibi ziko kwenye mtelemko unaopanda hadi mita 1800 kwenye mpaka wa jiji na mita 2000 juu ya UB kwenye nje ya jiji huko Limuru.

Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5°C mwezi wa Machi, na 16,8°C mwezi wa Julai. Wakati wa Juni na Julai usiku unaweza kuwa baridi halijoto ikishuka chini ya sentigredi 10.

Mvua nyingi hunyesha mwezi Machi (mm 199), kiangazi kina mm 14 tu wakati wa Julai.

Nairobi ya leo

Nairobi leo: New Central Bank Tower (140 m), Teleposta Towers (120 m), Kenyatta International Conference Centre (105 m), NSSF Building (103 m), I&M Bank Tower (100 m), Government Office Conference Hall (98 m).

Nairobi imeibuka kuwa mmojawapo kati ya miji mikubwa katika bara la Afrika. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbalimbali duniani.

Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa Nairobi hawakutegemea kuwa utatanuka hivyo. Wataalamu wengi wametoa maonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia wakazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka.

Nairobi imewavutia wakazi wengi, wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa wapo wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakaachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa Kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yoyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.

Kunayo pia matatizo ya ujambazi na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi.

Maeneo bunge

Kenyatta International Convention Centre na Times Tower.

Kaunti ya Nairobi imegawanywa katika maeneo bunge 17 na kata 85.

Tazama pia

Marejeo

  1. ↑ "Nairobi city County Hdi". Iliwekwa mnamo 2025-02-02.
  2. ↑ Christine Stephanie Nicholls, Red Strangers, uk. 37 f.
  3. ↑ Ukamba ilikuwa moja kati ya majimbo 4 ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (iliyokuwa koloni la Kenya tangu mwaka 1920) na makao makuu yalikuwepo Machakos
  4. ↑ Kituo cha polisi (Nairobi Central Police Station) iko mahali pa boma lile la kwanza
  5. ↑ ikaitwa baadaye Government Road, leo hii ni Moi Avenue
  6. ↑ Kama wale maarufu "Big Five" yaani tembo, simba, nyati, kifaru na chui
  7. ↑ www.iebc.or.ke Archived 19 Machi 2013 at the Wayback Machine

Viungo vya nje

  • Red Strangers: The White Tribe of Kenya, Christine Stephanie Nicholls, Timewell Press, 2005 (Google Books, imetazamwa Aprili 2 (Kiingereza)
  • Tovuti rasmi ya Nairobi Ilihifadhiwa 27 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
  • Chuo Kikuu cha Nairobi (Kiingereza)

web presence

reference

  • stated in / Marejeo ya URL 9
  • W imported from Wikimedia project 12
  • — 43

sw: 40 / 74

jamii kwa watu waliozaliwa hapa
Category:Births in Nairobi
category for people who died here
Category:Deaths in Nairobi
category of associated people
Jamii:Watu kutoka Nairobi
category for maps or plans
Category:Maps of Nairobi
category for the view of the item
Category:Views of Nairobi
topic's main category
Jamii:Nairobi
Wikipedia 211 ✓Wikivoyage 19Wikinews 5Wikiquote 3

87

archINFORM location ID8464
BabelNet ID00015561n
BBC News topic IDcq26565v4d9t
BBC Things IDbfe2de9d-fde7-4781-89ca-1735ede10982
BlackPast.org IDglobal-african-history/nairobi-kenya
BnF ID118650453
British Museum place IDx61211
Canadiana Name Authority IDncf10290894
CERL Thesaurus IDcnl00030086
Comic Vine ID4020-61168
Curlie IDRegional/Africa/Kenya/Localities/Nairobi/
Data Commons IDwikidataId/Q3870
Daum Encyclopedia IDb03n2669a
De Agostini IDNairobi
Dewey Decimal Classification2--67625
Encyclopædia Britannica Online IDplace/Nairobi
Encyclopædia Universalis IDnairobi
Facebook location ID114751268540391
FactGrid item IDQ449252
FAST ID1204373
FIPS 10-4KE05
France 24 topic ID (French)nairobi
Freebase ID/m/05d49
GeoNames ID184745
Getty Thesaurus of Geographic Names ID7001116
GitHub topicnairobi
GND4041172-2
GNS Unique Feature ID-2258072
Golden ID (archived)Nairobi-PJED
Google Maps CID17856493610344092236
Google News topics IDCAAqIQgKIhtDQkFTRGdvSUwyMHZNRFZrTkRrU0FtcGhLQUFQAQ
Gran Enciclopèdia Catalana IDnairobi-0
Gran Enciclopèdia Catalana ID (former scheme)0045300
Great Russian Encyclopedia Online ID (2017)2246269
Gynopedia IDNairobi
Harper's tagnairobi
HASCKE.NB
IdRef ID029153042
iNaturalist place ID10957
Interlingual Index IDi83637
ISNI000000010791732X
ISO 3166-2 codeKE-110
J9U ID987007552644805171
KBpedia IDNairobiArea-Kenya
Kitambulisho cha mamlaka ya Maktaba ya Bungen79011090
Le Figaro tag IDNairobi
Lex IDNairobi
Mapcarta IDNairobi
museum-digital place ID20868
MusicBrainz area ID4cc373f3-8b60-400b-8aa3-6df3fe4ab8fb
National Historical Museums of Sweden IDgeo/24610d81-9de7-4a91-97fc-9bb4cf1b8c7e
National Library of Spain SpMaBN IDXX453921
Naver Encyclopedia ID (pre-August 2026)1074255
NDL Authority ID00628843
NL CR AUT IDge432139
OmegaWiki Defined Meaning457020
Online PWN Encyclopedia ID3945429
OpenHistoricalMap relation ID2862891
OpenStreetMap relation ID9185096
OpenWeatherMap city ID184745
Proleksis enciklopedija ID38283
RKD thesaurus ID15689
SBN place IDTSAL000079
SNARC IDQ1381
Spanish Cultural Heritage thesauri IDgeografico/1150908
Store norske leksikon-IDNairobi
SVKKL authority ID0423566-Nairobi-Kena
Treccani IDnairobi
Treccani's Dizionario di Storia IDnairobi
Treccani's Enciclopedia Italiana IDnairobi
Tripadvisor ID294207
U.S. National Archives Identifier10044568
UK Parliament thesaurus ID11803
UN/LOCODEKENBO
VIAF264835402
Vikidia article IDfr:Nairobi
Vikidia article IDen:Nairobi
Vikidia article IDit:Nairobi
Vikidia article IDes:Nairobi
Who's on First ID421174401
WikiKids IDNairobi
Wikisimpsons article ID49149
WOEID1528488
WordNet 3.1 Synset ID08948355-n
WorldCat Entities IDE39PBJccgHVhXJcjCxQ6cXJxDq
YSO ID110125
‎Yale LUX IDplace/2594dec6-5ad7-4c29-9b82-864ef69905b3
Christine Stephanie Nicholls, Red Strangers, uk. 37 f.
Ukamba ilikuwa moja kati ya majimbo 4 ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (iliyokuwa koloni la Kenya tangu mwaka 1920) na makao makuu yalikuwepo Machakos
Kituo cha polisi (Nairobi Central Police Station) iko mahali pa boma lile la kwanza
ikaitwa baadaye Government Road, leo hii ni Moi Avenue
Kama wale maarufu "Big Five" yaani tembo, simba, nyati, kifaru na chui

Sources

  1. Christine Stephanie Nicholls, Red Strangers, uk. 37 f.
  2. Ukamba ilikuwa moja kati ya majimbo 4 ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (iliyokuwa koloni la Kenya tangu mwaka 1920) na makao makuu yalikuwepo Machakos
  3. Kituo cha polisi (Nairobi Central Police Station) iko mahali pa boma lile la kwanza
  4. ikaitwa baadaye Government Road, leo hii ni Moi Avenue
  5. Kama wale maarufu "Big Five" yaani tembo, simba, nyati, kifaru na chui
  6. www.iebc.or.ke Archived 19 Machi 2013 at the Wayback Machine

Composed by rule from Wikidata item Q3870 (composition/0.3, view/0.2, design/0.2). The lead paragraph, the section paragraphs and the section links come from Wikipedia. Pictures come from Wikimedia Commons; a W on a picture marks one from an article, not from Wikidata; a W on a value marks a statement whose only reference is a Wikipedia.

Add the label in sw